ITEL KUJA NA BIDHAA NYINGINE ZA KIELEKTRONIKI

Kampuni pendwa inayojali mahitaji na hali ya mwananchi wa kitanzania kwa muda mrefu sasa imekua ikitoa simu bomb ana za bei nafuu. Kwa miaka mingi sasa imekua ikiongoza kwa kuuza simu ambazo mtanzania wa hali yoyote ile anaweza kumudu kununua.

Sasa itel wameamua kuzidisha kusambaza upendo huo kwa kuwaletea wateja na wadau wake wa dhati bidhaa nyingine ili kufanya zoezi zima za kufurahia maisha liwe rahisi. Ukiachana na bidhaa nyingi ambazo itel wameleta, leo naomba nikufahamishe kwa ufupi kuhusu Laptop na TV za itel.

Zikiwa zimetengenezwa madhubuti kabisa kumlenga mtanzania, TV hizi za itel zimejaa rangi dhahiri, ambazo zipo vizuri kwa mng’aro. Mfumo wa TV ni wa kisasa uliowekwa ili kuonyesha maudhui ambayo macho ya mtazamaji yanatamani. Katika asili yake, huduma za televisheni dhamira yake ni kuwajulisha, kuelimisha, na kuburudisha. Kwa kulitambua hilo, bidhaa mpya za itel zinataka kufuata malengo hayo kwa kuwapa wateja vifaa bora vinayoenda na wakati.

Sambamba na TV, itel pia wameleta laptop kwa lengo la kuwafikia wanafunzi na watu ambao ni watumiaji wa kwanza wa laptop. Hii ilikua ni kwa ufupi tu, endelea kufuatilia kurasa zao za mitandao ya kijamii ili kujua zaidi kuhusu aina mbalimbali za TV pamoja na sifa za laptop yao

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s