BREAKING NEWS, (TAMISEMI) AJIRA ZA UALIMU 6949 NA AFYA 2726 ,2021 RASMI ZIMETANGAZWA NA WAZIRI UMMY MWALIMU.

Advertisements

The establishment of the Ministry of Regional Administration and Local Government is enshrined in the Constitution of the United Republic of Tanzania Articles 8 (1) 145 and 146 of 1977 and many other amendments that followed.

In 1982 the Union Parliament passed the District Authorities Act No 7 (Cap 287) and the Urban Authorities Act No 8 (Cap 288). These two Acts gave mandate to the Minister responsible for Local Authorities to establish Local Authorities in Districts, Villages, Urban Areas, Townships and Mitaa.

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA NA UALIMUOfisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) imepatakibali cha ajira za Watumishi wa Kada mbalimbali za Afya 2,726 kwa ajili yaHospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Walimu 6,949wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka zaSerikali za Mitaa nchini.Kwa sababu hiyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vyaUalimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutumamaombi yao ya nafasi za kazi kuanzia tarehe 09 – 23 Mei, 2021. Nafasi za ajirazilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) naShahada (Degree).

A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU

Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitiakiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz kwa utaratibu ufuatao: -i. Walimu wote wenye sifa ambao hawakuomba ajira za ualimu (tarehe07.09.2021) watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishicha ajira.tamisemi.go.tz;ii. Walimu walioomba ajira kwa njia ya mtandao kufuatia Tangazo la Ajira latarehe 07 Septemba, 2020, wanaelekezwa kuingia kwenye akaunti zaowalizotumia wakati wa kutuma maombi ili kuhakiki usahihi wa taarifa naviambatisho walivyotuma hapo awali; na2 | P a g eiii. Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2012hadi mwaka 2019.

2.0SIFA ZA WAOMBAJI2.1SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi wawe na Sifa za kitaaluma kamaifuatavyo:

2.1.1 WALIMU WA SHULE ZA MSINGI

Walimu wanaoomba kuajiriwa kufundisha Shule za Msingi wawe na Sifazifuatazo:

i.Mwalimu Daraja la IIIA:

Mhitimu wa Astashahada ya Ualimu Elimu yaMsingi, Astashahada ya Ualimu Elimu ya Michezo, Astashahada ya UalimuElimu ya Awali na Astashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum;

ii.Mwalimu Daraja la IIIB: 

Mhitimu wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu yaAwali, Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi na Stashahada yaUalimu wa Elimu Maalum; na

iii.Mwalimu Daraja la IIIC: 

Mhitimu wa Shahada ya Ualimu katika masomo ya“English Language, History na Geography”.

2.1.2 WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

i.Mwalimu Daraja la IIIB: 

Mhitimu wa Stashahada ya Ualimu wa Masomoya “Physics, Mathematics, Biology na Chemistry”;

ii.Mwalimu Daraja la IIIC: 

Mhitimu wa Shahada ya Ualimu aliyesomeaElimu Maalum kwa Masomo ya “Physics, Chemistry, Biology naMathematics”;

iii.Mwalimu Daraja la IIIC: 

Mhitimu wa Shahada ya Ualimu wa Masomo ya“Physics, Mathematics, Chemistry na Biology”; na

iv.Mwalimu Daraja la IIIC: 

Mhitimu wa Stashahada ya Uzamili katika Elimu(Post Graduate Diploma in Education) lazima awe mwenye Shahada yaKwanza (Bachelor Degree) yenye Masomo yaliyotajwa katika (ii) na iii)hapo juu. 

2.2. WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI

i. Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwakupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanzana Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezeshakuingia kwenye Mfumo wa Ajira; naii. Waombaji waliosoma Vyuo Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati yamasomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyaoviweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.

3.0 SIFA ZA JUMLA ZA MWOMBAJI WA AJIRA ZA UALIMU

Mwombaji wa nafasi zilizoainishwa hapo juu awe na sifa za jumla zifuatazo: -i. Awe ni Mtanzania;ii. Awe na umri usiozidi miaka arobaini na tano (45);

iii. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi waUmma;

iv. Awe na namba ya kitambulisho cha Taifa;v.Waombaji wenye Shahada na Stashahada za NACTE na TCU (UDOM)waambatishe Cheti cha Kuhitimu Mafunzo na “Transcript”. Waombaji waAstashahada na Stashahada za NECTA waambatishe Cheti cha Mafunzokatika sehemu mbili (weka cheti na weka “transcript”);

vi.Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne na Sita;vii.Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa; naviii.Maelezo Binafsi (CV), yakionesha umri, anuani kamili na namba ya simuya kiganjani.

B: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandaokupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz: –

2.0Sifa za Waombaji ni kama ifuatavyo:-

2.1DAKTARI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu kutoka VyuoVikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza Mafunzo yaKazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupataUsajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council ofTanganyika).

2.2DAKTARI WA MENO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu kutoka VyuoVikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza Mafunzo yaKazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupataUsajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council ofTanganyika).

2.3TABIBU DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in ClinicalMedicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwana Serikali.

2.4TABIBU MSAIDIZI

Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili yaTabibu Wasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Vyuovinavyotambuliwa na Serikali.

2.5TABIBU WA MENO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma inClinical Dentistry) ya muda wa miaka mitatu kutoka Vyuovinavyotambuliwa na Serikali.

2.6TABIBU MENO MSAIDIZI

Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya TabibuWasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwana Serikali.

2.7MFAMASIA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Famasi kutoka Vyuovinavyotambuliwa na Serikali waliohitimu Mafunzo kwa Vitendo(Internship) ya mwaka mmoja na ambao wamesajiliwa na Baraza laFamasi (Pharmacy Council).

2.8MTEKNOLOJIA (DAWA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa(Diploma in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka mitatukutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwana Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.9MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (DAWA)

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia waDawa ya Afya (Certificate in Pharmaceutical Technology) kwa mudawa miaka miwili kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali naambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.10 MTEKNOLOJIA (MAABARA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia waMaabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Sciences) kwamuda wa miaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali naambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya(Health Laboratory Practitioners’ Council).

2.11 MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA)

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia waMaabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Sciences) kwamuda wa miaka miwili kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali naambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya(Health Laboratory Practitioners’ Council).

2.12 MTEKNOLOJIA (MIONZI) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma inRadiology/Radiography) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Vyuovinavyotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza laWataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology andImaging Professionals Council).

2.13 MTEKNOLOJIA (MACHO) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Machokwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa naSerikali na ambao wamesajiliwa na Baraza lao.

2.14 AFISA MUUGUZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Vyuo Vikuuvinavyotambuliwa na Serikali, waliohitimu Mafunzo kwa Vitendo(Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza laUuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses and MidwiferyCouncil).

2.15 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Uuguzi, ya muda usiopunguamiaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali,waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TanzaniaNurse and Midwifery Council).

2.16 MUUGUZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katikaVyuo vinavyotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) naBaraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses andMidwifery Council).

2.17 MTOA TIBA KWA VITENDO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya miaka mitatu katika fani yaFiziotherapia/ Mtoa tiba kwa Vitendo kutoka Vyuo vinavyotambuliwana Serikali.

2.18 AFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira(Bachelor Degree in Environmental Health Science) kutoka Vyuovinavyotambuliwa na Serikali pamoja na Mafunzo kwa Vitendo(Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza laWataalamu wa Afya ya Mazingira (The Environmental HealthPractitioners Registration Council).

2.19 AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira yamiaka mitatu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali nakusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Afya ya Mazingira(The Environmental Health Practitioners Registration Council).

2.20 MSAIDIZI WA AFYA

Waombaji wawe wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu Mafunzo yaMwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii au mafunzoyoyote yanayofanana na hayo kutoka Vyuo vya Afyavinavyotambuliwa na Serikali.

2.21 KATIBU WA AFYA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya(Health Services Administration) kutoka Vyuo Vikuuvinavyotambuliwa na Serikali.

2.22 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada au Stashahada ya Juu (AdvancedDiploma) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Social Work, Sociology,Pscychology, Social Protection, Guidance and Counciling, Theology,Divinity, Child Protection, Social Policy, Any childhood development,Social Gelontology, au fani nyingine zinazofanana na Ustawi waJamii kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambuliwa na Serikali.

2.23 AFISA LISHE DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu naLishe, au Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc -8 | P a g eNutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science andTechnology, Food Science) au Stashahada ya Juu ya Lishe (HigherDiploma in Nutrition) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juuvinavyotambuliwa na Serikali.

3.0SIFA ZA WAOMBAJI KWA UJUMLA;

i.Awe raia wa Tanzania;

ii. Awe na umri usiozidi miaka 45;

iii. Awe na namba ya kitambulisho cha Taifa;

iv. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea;

v. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au asiwe Mwajiriwa wa Hospitali zaMashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali; navi. Asiwe mwajiriwa wa Serikalini au amewahi kuajiriwa Serikalini.

4.0MAOMBI YOTE YAAMBATISHWE NA NYARAKA ZIFUATAZO:

(i)Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne/Sita;

(ii)Nakala za Vyeti vya Taaluma;

(iii)Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa;

(iv)Nakala ya Cheti cha Usajili kamili (Full Registration) au Leseni yakufanya kazi ya taaluma husika; na

(v)Maelezo Binafsi

(CV), yakionesha umri, anuani kamili na namba yasimu ya kiganjani, pamoja na anuani/namba za simu za kiganjani zawadhamini wasiopungua wawili.

5.0MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

(i)Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauriwatakazopangiwa;

(ii)Waombaji wawe tayari kufanya kazi na Mashirika au Taasisizilizoingia Ubia na Serikali;(iii)Waombaji waliosoma nje ya nchi wanatakiwa waambatisheEquivalent Certificate kutoka NECTA/NACTE/TCU; na

(iv)Mara baada ya kupangiwa kituo cha kazi, hakutakuwa na nafasi yakubadilishiwa kituo cha kazi.

(v)Walimu wenye Ulemavu wenye sifa zilizoainishwa sawa na tangazo hiliwatume maombi yao ya kazi kwa nakala ngumu (hard copy) kwaSanduku la Posta, rejista au EMS. Maombi yao yaeleze aina yaulemavu wao na kuambatisha picha zao na yatumwe kwa anwaniifuatayo:

Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu,

S.L.P.980,

40480 DODOMA (Aione: Mkurugenzi wa Kitengo cha WatuWenye Ulemavu)
Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumajiwa maombi kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya:www.tamisemi.go.tz


Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwamoja Ofisini hayatafanyiwa kazi isipokuwa kwa Walimu wenye ulemavuambao maelekezo yao yametolewa katika kifungu cha 5(v). Mwisho wakupokea maombi ni tarehe 23 Mei, 2021 saa 5:59 usiku. Tangazo hililinapatikana katika tovuti ifuatayo: www.tamisemi.go.tzLimetolewa na: 

Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais – TAMISEMI,

Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P 1923,41185 DODOMA. 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s